Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Bituni Msangi amesema kuwa baadhi
ya walimu wa kike nchini hawavai mavazi yenye maadili ya ualimu hatua
ambayo huwasababisha wanafunzi hasa wa kiume kuwataka kimapenzi.
Picha hii hausiani na tukio ila ni mfano wa mwalimu akiwa Darasani
Msangi
ambaye pia kitaaluma ni mwalimu ametoa kauli hiyo kwenye hafla
iliyoandaliwa na Chama Cha Walimu (CWT) Wilayani Kongwa kwa ajili ya
kuwaaga walimu waliostaafu katika Wilaya hiyo.
Amesema
kuna baadhi ya walimu wa kike ambao wamekuwa wakikiuka maadili kwa
kuvaa mavazi mafupi na ya kubana wawapo kazini hali ambayo huwa
inawanyima wanafunzi wa kiume utulivu wa kujifunza ambapo amewaagiza
maofisa elimu kuwaeleza walimu wao namna bora ya uvaaji.
Katika
hafla hiyo jumla ya walimu 17 waliostaafu walipata zawadi ya mabati
20 kila mmoja waliyopewa na chyama cha walimu Wilayani humo.

No comments:
Post a Comment