Shirika
la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa virusi vya Zika ni dharura ya
afya ya umma ya kimataifa.
Tangazo
hilo limetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa WHO Margareth Chan
baada ya mkutano wa wataalam uliofanyika mjini Geneva Uswisi kujadili
mlipuko wa virusi vya Zika.
Mkurugenzi Mtendaji wa WHO Margareth Chan
Bi
Chan amewaambia waandishi wa habari kwamba uwezekano mkubwa wa
uhusiano kati ya virusi hivyo na tatizo la watoto kuzaliwa na vichwa
vidogo ni tukio lisilokawaida na linalohitaji jibu la kimataifa.
«
Wataalam wametilia maanani jinsi ugonjwa ulivyoenea hivi karibuni,
kadhalika jinsi mbu wanaoweza kuambukiza ugonjwa huu walivyoenea
duniani, ukosefu wa chanjo na vipimo vya mara moja, na ukosefu wa
kinga mwilini kwa watu wanaoishi katika nchi zilizoambukiwa hivi
karibuni, zote ni sababu za kutia wasiwasi zaidi. »
Dkt
Chan ameongeza kwamba bado WHO haijapendekeza vikwazo vyovyote dhidi
ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na ugonjwa huo, ila amesisitiza
umuhimu wa kujikinga na mbu kwenye nchi hizo.

No comments:
Post a Comment