Licha
ya serikali ya India kutangaza kuwa watu 5 wamekamatwa kwa kosa la
kuwashambulia na kumvua nguo mwanafunzi mmoja raia wa Tanzania, hofu
bado imetanda miongoni mwa takriban wanafunzi 150 wa chuo cha Acharya
Kaskazini mwa Bangalore .
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga
wawakilishi
wa wanafunzi hao wameiambia BBC kuwa uoga na hofu ya kutokea kwa
mashambulizi zaidi dhidi yao ndio imewafanya watanzania hao kukataa
kutoka makwao wakihofia usalama wao.
Hata
mkutano ulioitishwa na bodi inayosimamia chuo hicho cha Acharya
haukuhudhuriwa na wanafunzi kutokana na tishio la usalama wao.
Shambulizi
hilo liliwakumba wanafunzi wa kike raia wa Tanzania ambao bila ya
kujua kilichokuwa kimejiri walipita karibu na eneo ambalo mwanamfunzi
mmoja raia wa Sudan Kusini alikuwa amemgonga na kumuua mwanamke mmoja
mhindi
Hata
Hivyo Jana tayari serikali ya Tanzania imesema kuwa imeshapeleka
dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya India ili kuonyesha
kukasirishwa na kitendo hicho ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia
usalama wanafunzi hao raia wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment