Tanzania imesema haina mpango wa
kujitoa katika mahakama ya kimataifa ya ICC na kutaka kufanyiwa
marekebisho ya baadhi ya vipengele vinavyolalamikiwa kuwa haitendi
haki na imekuwa ikiwaonea viongozi wa bara Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu siku miamoja na serikali ya tano, waziri wa mambo ya nje,
ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kikanda na kimataifa balozi
Agustine Mahiga amesema ushindi wa rais wa Kenya na Bwana Uhuru
Kenyata na makamu wake William Ruto umedhihirisha kuwa waafrika
wanaweza kuishinda mahakama hiyo, na kusisitiza kuwa baadhi ya
vipengele vilivyowekwa lazima vitazamwe upya.
Waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kikanda na kimataifa balozi Agustine Mahiga
Aidha akizungumzia siku 100 za
serikali ya awamu ya tano, Balozi Mahiga amesema mafanikio mengi
yamepatikana katika kuimarisha siasa za kimataifa ikiwemo kuleta
maridhiano katika kulijadili mgogro wa Burundi, kuitangaza Tanzania
kimataifa pamoja na kuweka wazi misiamo ya Tanzania iliyosaidia kuwa
na nguvu ya pamoja na nchi marafiki katika kutatua changamoto
zilizopo nchni.
Aidha Balozi Mahiga amesema rais Dkt
John Pombe Magufuli anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kimatifa wa
marais wa nchi za Afrika Mashairiki unaotarajiwa kufanyika mapema
mwishoni mwa mwezi huu mjini Arusha, ambapo Tanzania ni mwenyekiti wa
mkutano huo unaolenga kujadili swala la kudumisha ushirikiano ndani
ya nchi wanachama na changamoto zinazojitokeza.

No comments:
Post a Comment