Ugonjwa wa ajabu umevamia mashamba
ya mahindi katika kijiji cha Chiwanda kata ya Nkangamo wilayani Momba
na kusababisha hasara kwa baadhi ya wakulima wa zao hilo kwakuwa
mashamba yaliyo na mimea iliyoathiriwa hayatawezaa kuzaalisha tena.
Afisa Kilimo wa halmashauri ya
wilaya ya Momba Oscar Mwilongo amesema ugonjwa huo unaosababisha
kukauka kwa mimea ya mahindi unahisiwa kuwa ule unaojulikana kwa jila
la kitaalamu la Maize Lathel Necrosis ambao ni hatari zaidi kwa zao
la mahindi.
Wakulima wakiwa wanavuna ndani ya shamba lao
Akitoa taarifa ya uwepo wa ugonjwa
huo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Momba kilichokuwa maalumu kwaajili ya kujadili Mapiti ya Bajeti ya
mwaka wa Fedha 2016/2017 Mwilongo amesema idara yake ilipata taarifa
ya ugonjwa Februari 19 mwaka huu.
Amesema baada ya kupokea taarifa
hizo aliongozana na timu ya wataalamu wengine na kufika kijijini
Chiwanda siku hiyo hiyo na kujionea athari za ugonjwa huo ambao
dalili zake zilionesha dhahiri ni ugonjwa wa Maize Lathel Necrosis.
Amesema Shamba la mkulima Innocent
Sanga lenye ukubwa wa Ekari tatu ndilo lililoathiriwa zaidi ambapo
baada ya kumhoji kwa undani alibainisha kuwa mbegu ya mahindi aina ya
Porp Corn aliyopanda kwenye shamba hilo aliletewa na kaka yake kutoa
Afrika Kusini.
Amesema baada ya majadiliano ya
wataalamu ngazi ya mkoa na vituo vya utafiti wa kilimo,hatua
zilizochukuliwa ni pamoja na Mahindi yote yaliyoathiriwa kung’olewa
na kuteketezwa kwa moto kabla ya kumalizika kwa juma hili na pia
mashamba yaliyokumbwa na ugonjwa huo hayapaswi kulima mahindi kwa
kipindi cha misimu mitatu mfululizo na badala yake yalime mazao jamii
ya kunde.
No comments:
Post a Comment