Idara ya uhamiaji mkoani Geita
inawashikilia raia 13 wa China kwa tuhuma za kufanya kazi za kutafiti
pamoja na kufanya kazi za kuchenjua madini ya dhahabu kinyume cha
sheria.
Watuhumiwa hao wamekamatwa katika
machimbo ya Igo katika kijiji cha Nyamahuna wilayani Geita kufatia
msako mkali kwa wageni wa mataifa kutoka nje wanaofanya kazi Mkoani
humo bila ya kuwa na kibali.
Raia wa china wakiwa Migodini Nkasi wakiwaendelea kufaya kazi
Akizungumza mara baada ya kuwakata
watuhumiwa hao Afisa Uhamiaji mkoa huo Charles Washima amesema
watuhumiwa hao waliingia nchini kwa kibali cha matembezi lakini
wamekua wakijihusisha na ufanyaji kazi kinyume na Sheria.
Nae Mmiliki wa Mgodi huo Bi. Rehema
Abdallah alishikiliwa na Idara hiyo baada ya kuhusika na kuwaleta
raia hao wachina kufanyakazi katika mgodi wake bila ya kuwa na kibali
maamulu.
No comments:
Post a Comment