Waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi profesa Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote wa wizara
yake mkoani simiyu kuwa waadilifu na atakayeshindwa kufanya hivyo
ataonyeshwa mlango wa kutokea kwa kupewa kilichochake ili kupisha
wanaohitaji kufanya .
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara
yake ya siku moja mkoani simiyu ya kukagua barabara ya Lamadi hadi
Bariadi yenye kilomita 71 ambayo iko katika hatua za mwisho
kukamilika na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami mwigumbi
Shinyanga hadi Maswa yenye kilomita 50.3 pindi alipokutana na
wafanyakazi wote walioko katika wizara yake
Waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi profesa Makame Mbarawa
Waziri amesema kuwa uadilifu katika
sekta ya miundombinu ni muhimu katika kuchochea kasi ya maendeleo na
hatimaye Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ,hivyo ni vema
wafanye kazi kwa bidii na ubunifu sambamba na kujiepusha na vitendo
vya rushwa.
Akiwa katika kambi ya kampuni ya
chicco inayojenga barabara ya mwigumbi maswa amemtaka mkandarasi
kufanya kazi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha kizuri na akifanya
kwa kiwango cha chini hatasita kumuondoa na kumtafuta mkandarasi
mwingine.
Aidha alitoa onyo kwa wafanyakazi wa
sekta ya mawasiliano kutojihusisha kuwa madalali wa makampuni
mengine, huku akitolea mfano kampuni ya TTCL na endapo akisikia mtu
anajihusisha na hilo lazima atamuondoa kazini.
No comments:
Post a Comment