Watu 3 wanaodhaniwa kujihusisha na
matukio ya kigaidi wameuwawa jana katika eneo la sinoni Engosheraton
mkoani Arusha baada ya kutokea majibizano ya silaha na Polisi
waliofika eneo la tukio kwaajili ya kuwakamata watu hao.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoani
Arusha kati ya watu hao ni mmoja pekee ambaye ametambuliwa kwa majina
ya Athumani Ramadhan Kassim mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni mzaliwa
wa Mkoani Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha
Liberarus Sabas amesema mtuhumiwa mmojawapo Athumani Ramadhan Kassim
alikamatwa baada ya taarifa za wasamari wema na kuwachukua polisi
hadi eneo la ENGOSHERATON-SINON kwaajili ya kuwaonesha walipo
wenzake, ndipo alipoanza kupaza sauti za “TAKBIR” na ghafla
wenzake wakaanza kuwarushia polisi risasi.
Polisi wanasema baada ya upekuzi
walikuta vifaa mbalimbali vya milipuko,kofia maalumu za kuficha uso
(MASK),sare 5 za jeshi la wananchi (JWTZ),vaz moja la mchezo wa
karete,pikipiki moja iliyobomolewa yenye namba bandia MC 983 BMK na
bendera 2 nyeusi zenye maandishi ya kiarabu zinazotumiwa na makundi
ya kigaidi.
Vitu vingine vilivyopatikana wakati
wa upekuzi ni kisanduku cha chuma,hati ya kusafiria ya NDUGU
Abrahaman Athuman Kangaa,simu tano za mkononi ambazo mojawapo
ilitambuliwa kuwa ni ya marehemu Mary Joseph aliyefariki kwa kupigwa
risasi na watu wasiojulikana mnamo tarehe 20/02/2016.
Adha Kamanda Sabas ameongeza kwamba
katika eneo la tukio pia wamekuta,kifurushi cha unga wa baruti,kisu
kimoja kikubwa,bunduki aina ya AK 47 na mafuta yake ya kusafishia
pamoja na magazine yenye risasi 18 lakini pia karatasi yenye maneno
ya vitisho kwa aliyekuwa kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam
Suleiman Kova.
Kwa upande wa wakazi wa Arusha
wametaka kuwemo na mkakati wa ziada kukabiliana na watu wahalifu wa
aina hiyo kabla hawajaleta madhara.
Miili ya marehemu hao imehifadiwa
katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwaajili ya uchunguzi na
utambuzi.
No comments:
Post a Comment