Jeshi la Polisi mkoani Mara
linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kumbaka kisha kunyongwa hadi
kufa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne na nusu Mariam
Deaogratus ambaye aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya awali ya makoko
katika manispaa ya Musoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara
kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ACP Philip Alex Kalangi, amesema
watu hao wamekamatwa siku moja tu baada ya kutokea kwa tukio hilo la
kikatili.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ACP Philip Alex Kalangi,
Awali kamanda alisema mtoto huyo
alikumbwa na mkasa huo muda mfupi baada ya kuondoka nyumbani kwao
jioni ya Februari 23 mwaka huu kwenda shule kwa ajili ya masoma ya
ziada, lakini akuonekana tena hadi saa 2 usiku wa siku hiyo Februari
23, mwili wake ulipokutwa ametupwa katika nyumba ambayo ujenzi wake
unaendelea.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Musoma, kamishina mwandamizi
mstaafu wa jeshi la polisi Zeloth Stephen, amesema vyombo vya dola
vitafanya kila Nnjia katika kuhakikisha mtu yoyote ambaye amefanya
kitendo hicho cha kikatili anakamatwa na kufikishwa mara moja katika
vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment