Watu wasiofahamika wamembaka mtoto
wa kike mwenye Umri wa miaka minne na nusu hadi kufa katika eneo la
Makoko Manispaa ya Musoma Mkoani Mara na kisha kuutupa mwili wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi Philip Kalangi
amesema mtoto huyo alikua akisoma katika shule ya awali katika shule
ya makoko katika Manispaa hiyo ambapo mwili wake ulikutwa katika
jengo ambalo halijakamilika ujenzi wake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi Philip Kalangi
Kamanda Kalangi amesema Polisi
wanaendelea na kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo lakini amewataka
wakazi wa maeneo hayo kukaa na kufikiria utaraibu wa kuwapeleka
watoto wao shule iki kuepusha majanga kama hayo kuendelea kutokea.
Akizungumzia juu ya tukio hilo baba
wa mtoto huyo amesema kuwa kawaida ya mtoto wao huwa anatoka shuleni
kwa saa nane na kisha kurejea shule saa tisa jioni kwa ajili ya
tuisheni lakini mama yake aliingiwa na wasiwasi baada ya mpaka saa
moja usiku mtoto alikua hajarudi nyumbani na ndipo alipotoa taarifa
na kuanza kumtafuta.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati
ya Ulinzi ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa wilaya ya Musoma Zelothe
Stephen amesema watu waliofanya kitendo hicho ni lazima wakamatwe
huku akiwataka wazazi kuwa waangalifu jinsi ya kuwapeleka na
kuwachukua watoto shuleni.

No comments:
Post a Comment