Mamlaka
ya Mapato nchini Tanzania(TRA), imeikabidhi Kampuni ya Udalali ya
Yono uwafilisi wateja 24 wanaodaiwa kodi ya shilingi Bilioni 18.95
baada ya kutorosha makontena ya mizigo kwenye bandari kavu ya (ICD).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Yono Kavela amesema hayo jana na kuongeza
kuwa wameowa amari na TRA, ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa na
kuwafilisi ili kulipa kodi wanazodaiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Yono Kavela
Bw,
Kavela amesema baada ya kupata kazi hiyo wameona ni busara kutangaza
na kuwapa siku 14 kulipa kodi wanazodaiwa na kwamba baada ya muda huo
kumalizika hatua za kukamata mazli za wadaiwa zitaanza.
Majina
ya wadaiwa hayo yametolewa jana kwa vyombo mbalimbali vya habari na
kampuni hiyo ya udalali baada ya TRA, kuwakabidhi kazi ya kuwafilisi
kutokana na kushindwa kutekeleza wajibu wao baada ya kupewa muda wa
kufanya hivyo.
Kavela
amesema ili kurahisha kazi Kampuni ya Said Salim Bakharesa ambayo
ndio mmiliki wa bandari kavu pamoja na kampuni ya Regional Cargo
Service wanapaswa kutoa ushirikiano kuhakikisha wadaiwa hao wanalipa
kodi walizokwepa.

No comments:
Post a Comment