Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),kimelalamikia kukamatwa kwa baadhi ya wabunge na madiwani
wao wa jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa kitendo hicho ni hujuma
zinazofanywa na watawala.
Akizungumza jana katika kikao cha
Kamati kuu ya Chama hicho Mwenyekiti wa taifa wa Chama hicho Mhe.
Freeman Mbowe ambapo amesema kuwa anahisi wakati viongozi hao
wakishikiliwa uchaguzi utaishwa wakati makada wao wakiwa kizuizini.
Mhe Mbowe amesema kuwa hatua ya
kukamtwa viongozi hao ni hujuma za kisiasa zinazoendelea ambapo pia
kumekua na mikakati ya kuzigawa manispaa wanazoziongoza ili Chama cha
Mapinduzi kiweze kuchukua nafasi katika Halmashauri Mpya.
Wabunge wanaoshikiliwa na Polisi
mpaka sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee. Mbunge wa
Ukonga Mhe. Mwita Waitara pamoja na madiwani wawili lakini pia Mbunge
wa Jimbo la Ubungo anaendelea kutafutwa na jeshi hilo kwa ajili ya
mahojiano zaidi.

No comments:
Post a Comment