Breaking News
recent

Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho nchini Tanzania(NIDA),imetangaza kusitisha mikataba ya Wafanyakazi 597

Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho nchini Tanzania(NIDA),imetangaza kusitisha mikataba ya Wafanyakazi 597 kwa muda kutokana na uzalishaji kuwa chini ya ufanisi usioendana na idadi yaxwafanyakzi walio nao.


Akiongea jana Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dkt. Modest Kipilimba amesema pia wafanykazi 802 wa kudumu ilionao inaendelea kwafanyia tathimini pia iwapunguze na kuwarudisha utumishi kwa kazi nyingine.
  
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa Mamlaka imekua ikizalisha vitambulisho 1200 kwa siku badala ya 24000 kwa siku jambo ambali ni sawa na uzalishaji wa wa chini ya asilimia kumi hivyo kuisabishia hasara mamlaka.


Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika uboreshaji wa utoaji wa vitambulisho hivyo wameongea na tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),ambao wamekubali kuwapatia mashine 5000,ambazo zilikuwa zinafanyiwa matengenezo.



Amesema kuwa mashine hizo zitsaidia kuongeza kasi ya kufikia wananchi wengi zaidi na kuwapatia vitambulisho lengo ikiwa ni kuhakikisha watanzania wote wanakuwa na vitambulisho vya taifa.
gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.