Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya Nne
Mhe. Mizengo Pinda ametoa wito kwa watumishi wa Umma kufanya kazi kwa
bidii na kuzingatia sheria na taratibu ili kuendana na kasi ya
serikali ya awamu ya tano ya kuwahudimia wananchi na kukabiliana na
umasikini.
Akizungumza wakati akifunga mkutano
kikao cha ushauri cha mkoa wa Katavi(RCC) ambapo amezishauri
halmashauri kufuata taratibu za manunuzi na matumizi ya pesa kwa
maslahi ya Umma ili kupiga hatua katika maendeleo ya mwananchi mmoja
mmoja.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Mizengo Pinda
Mhe. Pinda amesema licha ya kuwepo
kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa umma katika
utendaji wao ila amewataka watanzania kujenga tabia ya kutokukubali
kuwajibishwa kutokana na ukiukwaji wa utumishi wa Umma.
Aidha waziri Mkuu huyo Mstaafu
amewataka viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Katavi kuumunga mkono na
kumuombea rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi
ili kuleta maendeleo ambayo yalihidhiwa na watu wachache.
Mhe. Pinda ameongweza kuwa kwa
mwenzo wa Rais Magufuli anaamini kuwa ndani ya kipindi chake cha
miaka kumi kama akifanikiwa kumaliza vipindi vyote basi kutokana na
kasi yake Tanzania itakua imepiga hatua kubwa za kiuchumi na kuwa ni
moja kati ya nchi zenye uchumi wa kati.

No comments:
Post a Comment