Rais
Magufuli amesema kuwa amepanga kupangua upya mishahara mikubwa ya
wafanyakazi wanaopokea hadi shilingi milioni 40 na kusema kuwa lengo
lake ni kuhakikisha katika kipindi chake kusikuwepo watu wanaolipwa
zaidi ya shilingi milioni 15 kwa mwezi.
Ametolea
mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye
alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi
huyo atafikishwa mahakamani.
Pia
Rais Magufuli amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslai ya
wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi
asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo,
Rais
Magufuli amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo
inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu
cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15.
Kuhusu
tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo
uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa
wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na kwamba ni matarajio
kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini
wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za
watanzania.
Katika
hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa kila
mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa
misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti ambayo
inawanufaisha zaidi wao.
Dkt.
Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni
kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe
anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.
Akizungumza
na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
shule ya sekondari Chato, Wilaya ya Chato Mkoani Geita Rais Magufuli
amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu
serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma
wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa
hatua hizo zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.
No comments:
Post a Comment