Huduma
za matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula,
zilikosekana kwa muda baada ya madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo
kugoma kwa kushinikiza kutatuliwa kwa madai yao ikiwamo kuvitaka
vyombo vya ulinzi na usalama kuwatia nguvuni watu wanaodaiwa kumpiga
daktari wa hospitali hiyo, dkt. Dickson Sahini.
Wakizungumza
hospitalini hapo, baadhi ya wagonjwa wamesema kuwa toka wamewasili
hakuna huduma yoyote ya matibabu iliyotolewa kwao zaidi ya kupokelewa
mapokezi na kupatiwa cheti kisha kuambiwa wasubiri huku kukiwa hakuna
dalili zozote za kuhudumiwa.
Wakizungumza
mbele ya Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu, baadhi ya madaktari wa hospitali hiyo wamesema
kuwa hali ya usalama wao iko mashakani kutokana na kutokuwapo kwa
ulinzi wa kutosha hospitalini hapo huku wengine wakipata vitisho
kutoka kwa wananchi.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
Akitoa
tamkoa la serikali juu ya tukio la kupigwa kwa daktari, Mhe. Ummy
Mwalimu, amevitaka vyombo vya dola kutosita kuwachukulia hatua
wananchi wote wanaokwenda kinyume na matakwa ya sheria ili
kuwahakikishia watoa huduma za afya usalama na amani wakati wa
kutekeleza wajibu wao.
Aidha,
kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Henry Mwaibambe, amesema watuhumiwa wawili wanaodaiwa kutekeleza
tukio hilo tayari wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakani
haraka.
No comments:
Post a Comment