Serikali
ya Tanzania na Kuwait zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano katika
sekta ya usafiri wa Anga ambao utasaidia kupanua fursa za biashara
miongoni mwa nchi hizo mbili.
Akizungumza
katika utilianaji saini wa Mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Mkataba huo ni fursa
nzuri ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili ambapo Kuwait Airways
itaanza safari za moja kwa moja kutoka nchini humo kuja Tanzania.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
Aidha
Waziri Makame ameongeza kuwa licha ya ushirikiano wa kibiashara,sekta
hiyo ya usafiri wa anga itasaidia kukuza utalii wa Tanzania na
kuliongeza taifa pato kwa kiasi kikubwa.
Amesema
kuwa Mkataba huo pia unajumuisha mpango wa kubadilishanas uzoefu kati
ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA na Kuwait katika mafunzo
ya muda mfupi kwa watumishi wake.
Waziri
huyo amesema kuwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo ATC,itakua na
ndege mbili zinazotoa huduma za ndani ya nchi baadae nyingine
zitafanya safari katika ukanda wa Afrika Mashariki baadae nje ya nchi
ikiwemo Dubai, Kuwait na Bombay.

No comments:
Post a Comment