Shirika la Ugavi wa Umeme nchini
Tanzania (TANESCO),limewasilisha ombi la kutaka mabadiliko ya bei za
Umeme kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura).
Tanesco Imewasilisha Ombi hilo
ikitaka mabadiliko hayo ya umeme kwa asilimia 1.1 kuanzia tarehe moja
mwezi wa nne na asilimia 7.9 kwa mwezi January mwaka 2017.
Akitangaza kupokea maombo hayo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Nishati na Maji (Ewura), Felix
Ngalamgosi amekiri kupokea ombi hilo na kusema kuwa kwa sasa wako
kwenye utaratibu wa kukusanya maoni ya wadau ili waweze kufanya
mabadiliko hayo kutoka na mabadiliko ya uzalishaji wa nishati hiyo
nchini.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngalamgosi
Katika hatua nyingine Mkurugenzi
huyo ametangaza kushuka kwa Bei ya nishati za mafuta ya taa, Petroli,
na dizeli, baada ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia
huku akisema mabadiliko hayo hayatahusu mkoa wa Tanga.
Akitangaza bei elekezi jijini Dar es
Salaam Bw.Felix Ngamlagosi amewataka wateja wa nishati ya mafuta
kudai risiti pindi wanapopewa huduma hiyo na kwamba kuanzia sasa
wananchi wanaweza kupata bei hizo kupitia simu zao za kiganjani.

No comments:
Post a Comment