Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa - UNDP limetoa ripoti ya hali ya
maendeleo ya mwanadamu kwa mwaka uliopita, inayoonyesha kuwa Tanzania
bado inakabiliwa na changamoto kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira
na ajira bora kwa watu wake iwapo inataka kuboresha hali ya maisha
kufikia dira ya taifa ya mwaka 2030.
Mwakilishi
mkazi wa UNDP nchini Bw. Alvaro Rodrigues amesema kuna uhusiano wa
karibu kati ya ajira bora na maendeleo ya watu hivyo kuna haja ya
serikali kuwa na mipango inayotekelezeka ya kuboresha ajira na
mazingira ya kazi kwa watu wake.
Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Bw. Alvaro Rodrigues
Kwa
upande wake, Waziri wa Kazi, Ajira, vijana na walemavu Anthony
Mavunde amewataka waajiri kuheshimu sheria za kazi kwa kutoa mikataba
ya ajira kwa wafanyakazi wao huku wakitambua kuwa amani na usalama
ndio njia pekee inayoleta tija na ufanisi maeneo ya kazi.
No comments:
Post a Comment