Tanzania
imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia
(MCC) kusitisha msaada wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472.8
ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja pesa za Tanzania.
Waziri
wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga ameelezea mbele ya
Waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa
kushtushwa kwake na hatua hiyo ya bodi ya MCC ni kutokana na kupuuza
hatua kubwa tu zilizopigwa kidemokrasia nchini Tanzania.
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga
Kuhusiana
na uchaguzi wa Zanzibar Bw Mahiga anasema kuwa Tanzania, ilifanya
kila kitu kuambatana na sheria na katiba ya nchi wala hakuna tatizo
ama ukiukwaji wa sheria.
Mahiga
anasema kuwa huo ni uamuzi wao na kwa sababu hela hizo ni zao
wanauhuru wa kuzitumia watakavyo ila anahoji kwanini uamuzi huo
uliafikia bila ya majadiliano na serikali ya muungano ya Tanzania.
Waziri
huyo ameonya kuwa watu wanaoishi vijijini ndio watakaoathirika zaidi
kwani fedha hizo zilikuwa zimepangiwa kueneza umeme mashinani.
Katika
kutoa uamuzi wake, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC)
ilisema kuwa Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili
kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi
haitapokea msaada wa awamu ya pili.
No comments:
Post a Comment