Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Jenister
Joakim Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe uliotangazwa leo Jijini
Dar es salaam.
Taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa usiku huu, imeeleza kuwa uteuzi huo umetenguliwa kutokana
na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu.
ALIEKUA Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe
Kulingana na Taarifa hiyo, uteuzi
mpya kwa mujibu wa mamlaka na sheria utakapofanyika taarifa
zitatolewa kwa wananchi.
Mapema Jana waziri Muhagama alimteua
Dkt. Carina Wangwe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi
ya Jamii(NSSF) kuchukua nfasi ya Mkurugenzi wa zamani Bw. Ramadhan
Dau ambae aliteuliwa hivi karibu kuwa balozi.
No comments:
Post a Comment