Breaking News
recent

Zikiwa simesalia siku mbili kufanyika uchaguzi Mkuu wa marudio ya Uchaguzi Mkuu CUF, imetoa kauli ya mwisho ya kutoshiriki uchaguzi


Zikiwa simesalia siku mbili kufanyika uchaguzi Mkuu wa marudio ya Uchaguzi Mkuu CUF, imetoa kauli ya mwisho ya kutoshiriki uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Jumapili ya tarehe 20 Mwezi huu.


Akiongea akiwa mapumzikoni hotelini, Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa visiwani Zanzibar katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, huku akiwataka wananchama wa chame chake wasijitokeze siku ya upigaji wa kura.



Maalim Seif amesema kuwa msimamo wa upo pale pale na walishapelekea barua kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), pamoja na wagombea wote wa chama hicho ingawa tume hiyo bado imeyaweka majina yao katika karatasi za kura.



Aidha Maalim Seif amesema pamoja na tume kushinikiza uwepo wa ushikiriki wa lakini kamwe hawatoyatambua matokeo ambayo yatapitakana katika uchaguzi huo ambao unarejewa baada ya uchaguzi wa awali wa October 25 kufutwa na mwenyekiti wa tume hiyo kwa madai ya kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu Mkubwa.




Pia Katibu Mkuu huyo amelilalamikia Jeshi la Polisi Visiwani humo pamoja na Serikali kwa kuwakamata wanachama wa chama hicho bila sababu za msingi akiwemo katibu uenezi wa chama hicho visiwani humo na kusema CCM, hawapaswi kutumia nguvu kwa sababu uchaguzi huo utakua hauna upinzani wowote.
gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.