Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekemea
vitendo vya rushwa vinavyosababishwa ucheleweshwaji wa huduma ya
usafirishaji mipakani ikiwemo kwenye mipaka ya nchi ya Tanzania na
Rwanda.
Akizungumza
katika uzunduzi wa daraja la kimataifa la Rusumo linalounganisha
Tanzania na Rwanda jana katika ziara yake ya kikazi aliyoianza nchini
Rwanda rais Magufuli amesema kumekuwepo na vituo vya ukaguzi ambavyo
lengo lake ni kuchukua rushwa.
Rais
Magufuli amesema kuwa wingi wa vituo hivyo ulisababisha madereva
kukaa muda mrefu njiani ikiwa ni zaidi ya wiki huku akisema kwa sasa
anataka dereva asizidi siku tatu safari ya kutoka Dar es Salaam hadi
Rwanda.
Ameongeza
kuwa madereva wengi walikua wanachelewa kufika katika nchi hizo mbili
kutokana na adham wanazozipata ikiwemo rushwa ambapo amesema wengi
walikua wanatenga fedha za kutoa rushwa tangu mwanzo hadi mwisho wa
Safari.
Kwa
upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema Ujenzi wa daraja hilo
na kituo hicho utaimarisha uhisiano wa Tanzania na Rwada na amesema
anategemea nchi hizo zitafanya kazi kwa pamoja kwa kukuza maendeleo
endelevu
No comments:
Post a Comment