Mkuu
wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amewataka wanaomiliki silaha
za moto bila kuwa na vibali kuzisalimisha silaha hizo katika vituo
vya polisi ili kuepuka matumizi mabaya ya silaha yanayoweza kuchochea
vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.
Arusha
ni mkoa unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaomiliki silaha
kutokana na uwepo wa Wafanyabiasha wakubwa wakiwemo wafanyabiashara
wa madini ya vito aina ya Tanzanite.
Ntibenda
ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wenyeviti wa mitaa na
Watendaji wa serikali za mitaa katika wilaya ya Arusha mjini ambapo
amesema kuwa kwa sasa amesitisha kusaini vibali vya kumili silaha
mpaka pale zoezi la uhakiki wa silaha na usalimishwaj.
Mkuu
huyo wa Mkoa amepiga marufuku uuzwaji wa pombe aina ya viroba na
kuwataka viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana vyema na viongozi
halmashauri katika kusimamia maagizo ya serikali ili kusukuma
gurudumu la maendele.
Kwa
upande wao Wenyeviti wa Mitaa Jacob Meja Mwenyekiti wa mtaa wa Baraa
na Sara Mrema Mwenyekiti wa Majengo A wameiomba serikali iwaboreshee
mazingira ya kazi kwani wamekua wakikabiliwa na changamoto nyingi
ikiwemo kutolipwa posho na kutokua na ofisi.
No comments:
Post a Comment