Serikali
ya Tanzania imeweka bayana hatua tisa ambazo zitatumika katika kubana
matumizi ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Kuziba mianya ya
uvujaji wa fedha za umma na kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya
maendeleo.
Hatua
hizo zimetangazwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango, wakati akitoa taarifa kwa wabunge ya ukomo wa bajeti kuu ya
serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Dkt.
Mpango amesema katia ya hatua muhimu watakazochukua ni pamoja na
kufanya marekebisho ya sheria ya manunuzi ya Umma ili kuziba mianya
ya upotevu wa fedha katika manununuzi na kuhakikisha yanawiana na
thamani ya fedha itakayotumika.
Waziri
huyo wa fedha amesema hatua nyingine ni kukamilisha ni mchakato wa
kuziunganisha halmashauri zote nchini kwenye mfumo wa malipo ya
kibenki ili kuongeza udhibiti wa matumizi ya fedha za umma na
kufikisha malipo kwa wakati.
Aidha
Dkt. Mpango amesema hatuna nyingine muhimu pia ni kuhakikisha ,
wizara na idara zinazojitegemea, mikoa na mamlaka za serikali za
mitaa zinatumuia mfumo wa malipo wa serikali (IFMS), ili kuepuka
malimbikizo ya madai.

No comments:
Post a Comment