Jeshi
la Polisi Mkoani Arusha limeanza jitihada za kuwakamata watu
wanaohusika na mtandao wa kuchoma moto shule za Bweni ,kufuatia
mfululizo wa matukio ya shule za Bweni 6 kuteketezwa kwa moto siku za
karibuni.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha
Charles Mkumbo, amesema kuwa majira ya saa 8 usiku tukio linguine la
kuteketea kwa moto bweni la shule ya sekondari Winning Spirit mkoani
Arusha limetokea ,chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kwani
uchunguzi unaendelea.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
Kamanda
amesema kuwa tayari watumiwa 27 wanashikiliwa na jeshi hilo kwa
kuhusishwa na matukio hayo ya moto na hatua zaidi zinachukuliwa
kuhakikisha kuwa Wahusika wote wanabainiwa na kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria..
Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la zima moto na Uokoaji mkoani Arusha Bakari
Mrisho amesema kuwa kikosi chake kimefanya uchunguzi katika shule
tano za bweni zilizoungua awali na kujirishisha kuwa ni hujuma za
kibinadamu zimesababisha kuungua kwa mabweni hayo na kwasasa
wamejielekeza kufanya ukaguzi katika shule za bweni na kuangalia
iwapo zina uwezo wa kukabiliana na majanga ya moja.
Kwa
upande wao wananchi wa Arusha Zakia Hassan na Patrick Samwel
wameitaka serikali kuimarisha ulinzi katika shule za bweni ili
kuepuka changamoto za mabweni kuungua moto.
Tayari
shule sita mkoani Arusha zimekumbwa na janga la moto ikiwemo shule
ya Sekondari Winning spirit,Lowasa sekondari,Nanja sekondari,Sokoine
sekondari ,Longido sekondari pamoja shule ya sekondari
Mlangarini.Juhudi za serikali na vyombo vyake zinahitajika kukomesha
matukio hayo ya shule kuungua moto.
No comments:
Post a Comment