Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),wameahirisha Maandamano ya
kupinga kile wanachokiita wao ni Udikteta Uchwara (UKUTA),ya nchi
nzima ya kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa ya viongozi wa dini na
taasisi nyingine za amani na haki za binadamu kukaa na rais John
Magufuli ili kulitatua suala hilo.
Akiongea
kuhusiana na tamko hilo rasmi Mwenyekiti wa Chadema,Mhe. Freeman
Mbowe amesema wamefikia hatua hiyo ya kuahirisha UKUTA lakini
wamewataka wanachama wao kuendelea kusikiliza kauli za viongozi hao
mpaka pale watakapo toa mwongozo mwingine kuhusiana na madai yao.
Mwenyekiti wa Chadema,Mhe. Freeman Mbowe
Mbowe
amesema licha ya Chadema kuwasikiliza Viongozi wa dini lakini CCM na
serikali yao wao wamejipanga kufanya mapambano na viongozi wa Chadema
na raia ambao wanataka kudai haki yao.

No comments:
Post a Comment