Shirikisho
la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA, limesema kuwa haliungi mkono
kusudio la baadhi ya vyama kufanya maandamano kinyume na utaratibu
uliowekwa kisheria.
Katibu
Mkuu wa TUCTA, Nicholaus Mgaya amewaambia waandishi wa habari mkoani
Dodoma, amesema kuwa Shirikisho hilo limeundwa kwa ajili ya kutetea
wafanyakazi na kamwe halijihusishi na masuala ya kisiasa.
Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholaus Mgaya
Mgaya
amesema kuwa Shirikisho hilo linaundwa na wajumbe wenye itikadi ya
vyama tofauti lakini falsafa na sheria ya kuundwa kwa shirikisho hilo
ni pamoja na kutojihusisha na masuala yoyote ya kisiasa kwa maslahi
wa watu fulani.
Aidha
Mgaya amesema licha ya kusimamia haki za kwa wafanyakazi lakini pia
kusemea jamii kwa mambo ambayo hayaendi vizuri lakini pia kuishauri
serikali ni jinsi gani ya kubana matumizi kwa ajili ya kujenga uchumi
wa nchi kupitia wafanyakazi.
Katika
hatua nyingine Mgaya amesema kuwa shirikisho hilo limepongeza hatua
ya serikali kurudisha makao makuu ya nchi Mkoani Dodoma na kusema
uamuzi huo utaotoa fursa kwa uchumi wa mkoa kukua kwa kasi.

No comments:
Post a Comment