Watanzania
wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda kupima afya zao mara kwa mara
pamoja na kuepuka ngono zembe ili kuepuka maambukizi mapya ya homa ya
ini ugonjwa ambao tiba yake mpaka sasa bado ni changamoto.
Hayo
yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Afya kutoka Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania, Dkt. Goodluck Moshi, ambapo amesema kuwa serikali
inatakiwa kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya madhara ya ugonjwa
huo pamoja na kujikinga na maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Dkt
Moshi amesema kuwa taifa sasa linatakiwa kujipanga kuanzia mashule na
kuweka mtaalamu maalumu unaoelezea homa ya Ini lakini pia vyombo vya
habari pamoja na mahospitali kwa kufanya hivyo nchi inaweza kuzuia
kwa kiasi kikubwa kuenea kwa ugonjwa huo.
Aidha
amesema kuwa serikali inatakiwa kusisitiza kupata chanjo kuanzi kwa
watoto pamoja na watu wazima ingawa upatikanaji wake una gharama za
juu lakini haina budi kufanyika jitihada za kupatikana kwa njacho
hiyo ili kujikinga na ugonjwa huo hatari.

No comments:
Post a Comment