Breaking News
recent

ILO linakadiria kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana kimataifa utazidi kupungua kwa mwaka 2016

Shirika la kazi duniani ILO linakadiria kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana kimataifa utafifikia asilimia 13.1 mwaka huu wa 2016 na kusalia katika kiwango hicho hadi mwaka 2017.

Ripoti ya Mtazamo wa kimataifa wa ajira na kijamii 2016 ikiwalenga hasa vijana , inaonyesha kwamba idadi ya vijana wasiokuwa na ajira itaongezeka kwa nusu milioni mwaka huu na kufikia milioni 71 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kushuhudia ongezeko hilo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Jenista Mhagama
ILO inasema cha kusikitisha zaidi ni idadi yay a vijana hasa katika nchi zinazoendelea ambao wanaishi katika hali ya umasikini ama wa wastani au wa kupindukia licha ya kuwa wanafanya kazi.


Takwimu zinaonyesha kuwa vijana milioni 156 asilimia asilimia 33.7 wanao fanya kazi wako katika hali ya umasikini ama wa wastani au wa kupindukia ikilinganishwa na asilimia 26 ya watu wazima wanaofanya kazi.
gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.