Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewaagiza viongozi wote wa kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitongoji
nchini mwake kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali
kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo la kudhibiti mianya ya
matumizi mabaya ya fedha hizo.
Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na
Buseresere Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Katika
agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya
udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi
halisi kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema
Serikali itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya
hivyo.
"Ninafahamu
mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo,
wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika
shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi
waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii
ina wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki
tano, za wanafunzi laki moja wagawane.
"Napenda
nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia
mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali" Amesema
Rais Magufuli.
Pamoja
na agizo hilo, Rais Magufuli pia ametaka viongozi wa ngazi zote
katika Mikoa kuhakikisha wana takwimu za idadi ya wanafunzi katika
shule zote zilizopo katika maeneo yao ili kurahisisha ufuatiliaji wa
fedha hizo na amesema kuwa kuanzia sasa ataanza kutembelea shule kwa
kushitukiza na kwamba kiongozi atakayeonekana kutojua takwimu itakuwa
ni uthibitisho kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa alionao.
"Na
nitoe wito kwa viongozi wa Mikoa, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi, Makatibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji,
kila mmoja awe na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule zao,
hatutaki kuwapunja wanafunzi hela ambayo wanatakiwa kupata, lakini
pia hatutaki kutoa hela ambayo haitakiwi" Amesisitiza Rais
Magufuli.
Mhe.
Rais Magufuli ambaye ametumia mkutano huo kueleza juhudi mbalimbali
zilizofanywa na Serikali yake ya Awamu ya Tano, kutekeleza ahadi yake
ya kujenga Tanzania Mpya pia amewataka viongozi na watendaji wa
Serikali kutekeleza wajibu wao kwa kutembelea wananchi wanaowaongoza
badala ya kukaa muda mwingi ofisini huku akisisitiza ofisi hizo
kuwepo katika maeneo yenye shughuli husika.
Aidha,
Dkt. Magufuli amekosoa utaratibu unaotumiwa na Halmashauri nyingi za
Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kutumia mawakala katika ukusanyaji
wa mapato ya Halmashauri akisema mawakala hao wamekuwa wakitumia
utaratibu huo kukusanya fedha nyingi na kisha kuwasilisha kiasi
kidogo katika Halmashauri husika.
"Hivi
kwa nini Halmashauri msingekuwa na maafisa wenu wazuri na mkawa na
mashine za kielektroni kwa ajili ya kukusanya fedha? Amehoji Dkt.
Magufuli na kuongeza kuwa "tena mawakala wengine ndio hao hao
wamekuwa wakikusanya kodi hata kwa wananchi wanyonge wenye vibiashara
vidogo vya kuuza mchicha bila hata kuwaonea huruma"
Rais
Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amemaliza
ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na
Geita na yupo nyumbani kwake Chato Mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.

No comments:
Post a Comment