Mahakama
nchini Tanzania imejipanga kurejesha imani ya wananchi kwa mhimili
huo muhimu katika utoaji wa haki kwa kuhakikisha uwazi na uwajibikaji
pamoja na kupokea malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi kwa
wakati.
Hayo
yameelezwa Yameelezwa na Mtakwimu wa Mahakama ya Tanzania Idara ya
Mipango na Ufuatiliaji Mcharo Mwanga na Naibu Msajili wa Mahakama ya
Arusha Augustine Rwizile wakati wa kikao kazi cha kutoa elimu ya
Mpango Mkakati wa Mahakama wa mwaka 2015/16-2019/2020.
Mtakwimu wa Mahakama ya Tanzania Idara ya Mipango na Ufuatiliaji Mcharo Mwanga
Aidha
wamesema kuwa Mpango huo utasaidia Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi
na kupokea mrejesho kutoka kwa wananchi kupitia Simu Maalumu za
kupokea Malalamiko ya Wananchi juu ya uendeshaji wa shughuli za
mahakama.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jaji Fatuma Msengi amesema
kuwa mpango mkakati huo utasaidia kuboresha mahusiano kati ya
mahakama na wadau na pia kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema kuwa suala la haki
sawa na uwajibikaji wa mhimili wa Mahakama pamoja na uwazi litasaidia
katika utendaji wa kila siku wa mahakama.
No comments:
Post a Comment