Mwanafunzi
wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya jamii katika Chuo Kikuu cha
Dodoma (Udom), Fredrick Joseph (25), ameuwawa kwa kushambuliwa kwa
kipigo na watu wanaosadikiwa kuwa ni wanafunzi wenzake wakati akitoka
klabu ya pombe (Bar).
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Chuo hicho
ambapo Mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi
wakafika na kumkuta akiwa anagalagala njiani.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa,
amesema Mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara
alishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na watu
wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa,
Amebainisha
mwanafunzi huyo alikutwa majira ya saa 10 alfajiri katika eneo hilo
la Chuo hicho huku akisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa
marehemu huyo alikuwa na ugomvi na watu hao katika klabu ya pombe ya
Canival Pub iliyopo chuoni hapo.
“Alipoondoka
kurudi bwenini akiwa njiani alishambuliwa na watu hao wasiofahamika
na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, Kipigo
kilichosababisha kifo chake wakati alipokimbizwa kutibiwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Dodoma,”alisema Mambosasa
Amesema
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali hiyo kwa uchunguzi
zaidi na hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Alipoulizwa
kuwa taarifa za mwanafunzi huyo kushambuliwa na wenzake, Mambosasa
alisema kwasababu inadaiwa haifahamiki upelelezi bado unaendelea.
“Kwa
sababu mwenye bar si yupo, kama kuna ugomvi ambao ulikuwa unaendelea
tutajua tu, nimemuelekeza OCD kufuatilia ni nani waliokuwa wanakunywa
kwenye hiyo bar chuoni, ni lazima tu watakuwa wanachuo ili
tuwabaini,”
Kamanda
huyo amesema ameelekeza uchunguzi wa kina ufanyika kama kulikuwa na
ugomvi ndio hao hao walienda kumtegea njiani.
Chanzo
cha habari ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye siyo
msemaji wa polisi amesema kuwa marehemu Joseph alikuwa anakunywa
pombe pamoja na marafiki zake lakini baada ya kulewa walianza ugomvi
ambao hata hivyo waliamuliwa.
“Baada
ya kuamuliwa ule ugomvi wa awali ndipo wenzake walipokwenda
kumsubiria kwa mbele kwenye kichaka ambapo walimvamia na kumshambulia
na kumwacha karibu ya kufa,” kilisema chanzo hicho.
Ameongeza
kuwa, baada ya kumwacha hapo na kutoweka ndipo walinzi wa chuo hicho
waliokuwa doria walimwokota na kumfikisha kwenye kituo kidogo cha
polisi kilichopo Chimwaga ambapo alikimbizwa katika hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipofariki wakati akipatiwa matibabu.
Amesema
hakuna mtuhumiwa hata mmoja anayeshikiliwa na polisi kwa kuwa wote
waliomshambulia walitoroka na hawajulikani walipo.
No comments:
Post a Comment