Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo cha polisi cha kati jijini hapa aliyetambulika kwa jina la Victoria Wenga mwenye umri (51) mkazi wa Lemara jijini Arusha amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia leo kwa kutumia shuka lake ndani ya mahabusu , bila kuacha ujumbe wowote.
Marehemu alikamatwa Agosti 21 mwaka huu majira ya Alfajiri kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba yake na maduka yake mawili kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa chanzo cha mtuhumiwa kujinyonga bado akija fahamika ila mtuhumiwa alikuwa akishikiliwa kwa kosa la kuchoma moto mali zake.
kamanda wa polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo
Kamanda mkumbo amefafanua kuwa kugundulika kwa tukio hilo kulitokana na kelele za mahabusu wenzake kubaini tukio hilo na ndipo mkaguzi wa mahabusu alipo fika na kushuhudia mwili wa marehemu ukiwa unaning'inia katika mahabusu hiyo.
Marehemu Victoria anadaiwa kuwa na ugomvi wa kifamilia na mume wake aliye tambulika kwa jina la Edward Wenga akimtuhumu kuzaa nje ya ndoa kinyume na utaratibu
Hatua ya ugomvi huo imeelezwa kuwa chanzo cha marehemu kufikia hatua ya kuteketeza mali walizochuma na me wake maduka mawili na nyumba ya kuishi
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali ya Mount Meru.
Mwisho
No comments:
Post a Comment