Serikali
imewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha inashirikiana na
wadau mbalimbali wa maendeleo ili kutatua changamoto ya ukosefu wa
matundu ya vyoo iliyopo.
Naibu
waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa
SULEIMAN JAFO amesema hayo leo mjini Dodoma katika kikao cha kamati
ya utawala na serikali za mitaa kwa ajili ya kutatua kero ya ukosefu
wa madawati na miundombinu mingine katika sekta ya elimu.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa SULEIMAN JAFO
Amesema
jambo hilo ni la siku nyingi na linatia aibu na serikali peke yake
haiwezi kukamilisha mahitaji yote ya matundu yaliyopo hivyo ni vyema
wakuu hao wakashirikisha wadau ikiwemo nguvu kazi ya wananchi.
kwa
upande wake mkurugenzi msimamizi wa elimu ofisi ya rais TAMISEMI JUMA
KAPONDA amesema mahitaji ya matundu ya vyoo upande wa shule ya
msingi ni 44,517 ambapo yaliyopo ni laki 162,754 na hivyo kuwepo wa
upungufu wa matundu lajki 248,763.
Upande
wa shule za sekondari mahitaji ni matundu elfu 42,365 wakati matundu
yaliyopo ni 23,571 idadi ambayo inafanya uwepo wa upungufu wa matundu
elfu 18,784.
KAPONDA
amesema serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2016/2017 katika mapato
ya ndani ya halmashauri imetenga jumkla ya shilingi bilioni 10.1 kwa
ajili ya kujenga matundu ya vyoo elfu 8,791 katika shule za msingi na
kwa shule za sekondari imetenga shilingi biliobi 2.5 kwa ajili ya
ujenzi wa matundu elfu 1,942.

No comments:
Post a Comment