Waziri
Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewataka vijana kuendana na kauli mbiu ya
Serikali ya hapa Kazi tu ili iweze kuleta tija kutokana na Uchumi wa
nchi unategemea zaidi mchango wa vijana katika shughuli mbalimbali za
maendeleo.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema hayo jana wakati akifungua Maonesho ya 24 ya
wakulima maarufu kama nane nane kwa kanda ya Mashariki yaliyofanyika
mkoani Morogoro katika viwanja vya mwalimu Julias Kambarage nyerere.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa,
Mhe.
Majaliwa amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea zaidi kilimo hivyo
amewataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufanya kilimo
chenye tija kwao na taifa kwa ujumla na kufikia malengo yaliyowekwa
na serikali.
Aidha
Waziri Mkuu amesema kuwa kutokana na mkoa huo na matukio mengi ya
migogoro ya wakulima na wafugaji serikali imeweka suluhisho ambalo
litakua la kudumu ikiwemo kugawa vitalu kwa wakulima na wafigaji.

No comments:
Post a Comment