Wafanyabishara
katika standi ndogo ya Arusha wameandaman hadi ofisi za halmashauri
wakishinikiza kupewa mikataba ya maduka wanayopangisha wanayodai
kuwa swala hilo limekuwa likipigwa danadana na ungozi wa jiji la
Arusha.
Awali
halmashauri ilitoa viwanja kwa wafanyabiashara ikiwataka kujenga na
kutumia maduka hayo kwa kipindi cha miaka kumi bila kuilipa chochote,
na baadae kukabidhi maduka hayo kwa halmashauri ya jiji..
Wafanyabiashara
hao wameeleza kuwa sasa wamekuwa wakifanyabishara zao kwa wasiwasi,
kufuatia mkanganyiko wa kimasilahi kati ya madalali wa maduka yao na
halmashauri.
Kufuatia
maelezo hayo Meya wa jijji la Arusha Kalisti Lazaro akalazimika kutoa
maelelekezo ya namna yaulipaji huku akieleza kuwa tatizo kubwa ni
madalali hao wamekuwa wakisababishia serikali upotevu wa mabilioni
ya fedha kwa kutolipa mapato.
Meya wa jijji la Arusha Kalisti Lazaro
Mstahiki
meya amewataka wafanyabiashara hao kuendelea na majukumu yao huku
akiwahakishia kuwa swala la mikataba linafanyiwa kazi katika kipindi
kifupi .
Wakati
mgogoro huo ukifukuta tayari duka moja limedaiwa kuvunjwa huku sababu
kubwa ikidaiwa kuwa kushindwa kulipa kodi kwa halmashauri ,huku
muhusika akidai amelipa kodi yake yote kwa mmilikiwa wa duka hilo.
No comments:
Post a Comment