Kufuatia
hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa
mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali
kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Waziri
Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Bw.
Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo
tarehe 23 Septemba, 2016 huku aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL
Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.
………………………………...
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto nchini Tanzania (UNICEF) na
serikali wamezindua hatua mpya ya usajili wa watoto wote wanaozaliwa
na walio na umri wa chini ya miaka mitano mradi huo ulioanza mwaka
2012 kwa majaribio una lengo la kufikia mikoa yote ya Tanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kampeni hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Dk.
Harrison Mwakyembe amesema hadi sasa watoto 400,000 wameshasajiliwa
na kupewa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa ya Mbeya na Mwanza na sasa
kampeni hiyo imeingia mikoa ya Iringa na Njombe.
………………………………....
Shirika
la Afya Ulimwenguni (WHO), leo limezindua mkakati wa kukabiliana na
magonjwa ya moyo yakiwamo shambulio la moyo na kiharusi, magonjwa
yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani.
Kwa
mujibu wa WHO, zaidi ya watu milioni 17 hufariki dunia kila mwaka
kutokana na magonjwa ya moyo, wengi wa wanaofariki hugundulika
kutumia tumbaku, kula vyakula vyenye chumvi nyingi, na kutofanya
mazoezi ambapo shirika hilo limesema wengi wanaweza kuokolewa kwa
kupatiwa tiba mbalimbali.
..
.................................................
Maafisa
polisi wawili wameripotiwa kutojulikana walipo baada wapiganaji wa
Al-Shabaab kushambulia kambi yao ya Hamey katika kaunti ya Garissa
nchini Kenya.
Msemaji
wa jeshi la polisi Kenya, George Kinoti amesema washambualiaji hao
wameiba bunduki aina ya machine gun, risasi 1,000 pamoja gari aina ya
Toyota Land cruiser.
…..............................................
Manusura
wa bodi iliyozama kwenye eneo la karibu na Pwani ya Misri, wamesema
kuwa mamia ya watu huenda wamekufa maji.
Boti
lililozama lilikuwa limebeba kati ya watu 450 ama 600 ambao ni
wahamiaji ilipozama kilomita 12 kutoka ufukwe wa Misri.
…………………….................
Na,
Utafiti
uliofanywa nchini Uingereza umebaini kuwa wanawake wengi
wanofanyakazi wamekuwa wakipata maumivu ya makali wakati wa hedhi,
ambayo yamekuwa yakiathiri uwezo wao wa kufanyakazi.
Utafiti
huo uliofanywa kwa wanawake 1,000 umebaini kuwa asilimia 52 kati yao
hupatwa na maumivu makali ya hedhi, lakini ni asilimia 27 tu
walioweza kuwaambia mabosi wao kuwa ufanisi wao umeathiriwa na
maumivu hayo.
Goza News

No comments:
Post a Comment