Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitumia
salamu za rambirambi familia ya Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam
Dkt. Didas Masaburi aliyefariki dunia jana tarehe 12 Oktoba, 2016
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Katika
salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea taarifa ya kifo cha Dkt.
Didas Masaburi kwa mshituko na masikitiko makubwa na kwamba anaungana
na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki
kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.
Aliewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi
"Poleni
sana familia ya Dkt. Didas Masaburi, najua huu ni wakati mgumu sana
kwenu, lakini niwahakikishie kuwa sote tumeguswa sana na msiba huu
kwa kuwa tumempoteza mtu muhimu, msomi mzuri, kiongozi aliyelitumikia
Taifa kwa moyo wake wote na aliyesimamia kile alichokiamini"
amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.
Aidha,
Dkt. Magufuli amewapa pole wanachama na wapenzi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ambao wamempoteza Mwana CCM mwenzao pamoja na
Viongozi na watumishi wa Jiji la Dar es Salaam ambao walifanya nae
kazi alipokuwa Meya wa Jiji.
Amemuombea
kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi.
"Bwana
alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina" amemalizia
Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment