Breaking News
recent

Tanzania,DRC watiliana saini kuimarisha Ushirikiano


Tanzania,DRC watiliana saini kuimarisha Ushirikiano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimakribisha Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), wametiliana saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali ikiwemo suala la Ulinzi na Usalama pamoja Uchimbaji wa Mafuta katika ziwa Tanganyika.
Akiongea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais Joseph Kabila, Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekubaliana ushirikiano wa kimaendeleo katika uwekezaji pamoja jinsi ya kusimamia uchaguzi ujao wa nchi hiyo kupitia uongozi wake katika nchi za Jumuiya ya nchi za SADC.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa mbali ya kuangalia masuala ya kiusalama nchini humo lakini pia amemuomba wafanyabiashara kutoka nchini Congo kuja kuwekeza nchini pamoja kutumia bandari ya Dar es salaam kwa katika usafirishaji wa bidhaa.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Joseph Laurent Kabila amesema kuwa anaamini ushirikiano huo utakuza maendeleo ya pande zote mbili pamoja na nchi za jumuiya ya (SADC) ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi utakaozingatia Demokrasia nchini humo.

Samia Suluhu Hassan leo, amefungua Mkutano wa 30 wa Kisayansi

Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo, amefungua Mkutano wa 30 wa Kisayansi Jijini Dar es Salaam, uliowakutanisha watunga sera, wataalamu wa afya kutokana nchi mbalimbali duniani kujadili namna ya kutatua changamoto mbalimbali za magonjwa kupitia tafiti za kisasa.
Mhe. Samia amesema mkutano huo pamoja na mambó mengine utajadili namna ya kushughulikia uzazi wa mpango, na urahisi wa kufikia huduma za afya na namna ya kuondoa changamoto za huduma za afya kupitia tafiti na kukuza maendeleo endelevu.

Magufuli, amempongeza Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro kwa kuteuliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amempongeza Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro kwa kuteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mkuu wa Ofisi ya Umoja huo Sudan Kusini.
Katika pongezi hizo Rais Magufuli amesema Tanzania imepokea uteuzi huo kwa heshima kubwa na ipo tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitaji kwa Balozi Joram Mukama Biswaro katika utekelezaji wa majukumu yake.

Asilimia tano ya watoto katika mataifa yanayoendelea wanaishi katika umasikini

Benki ya Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto, wamesema karibu asilimia tano ya watoto katika mataifa yanayoendelea wanaishi katika umasikini uliokithiri.
Watoto hao ambao idadi yao inafikia watoto milioni 385, wapo katika kaya ambazo kipato chake kinafikia dola 1.90 ama chini ya hapo kwa siku, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.