Siku
chache baada ya kutokea tukio la kushambuliwa mwanafunzi ikiwa kama
adhabu mkoani Mbeya, waalimu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi
mkoani Njombe baada ya kudaiwa kumshambulia mwanafunzi wa kike wa
kidato cha nne kwa kosa la kukutwa simu ya mkononi katika begi lake
la chuma la nguo na waalimu wake.
Mwanafunzi
huyo wa shule ya binafsi ya sekondari ya Mbogamo, ya mkoani Njombe,
Elizabeth Simfukwe anadaiwa kushambuliwa na mkuu wa shule akiwa na
waalimu wengine na kumsababishia maumivu kisha kulazwa katika
Hospitali ya Kibena mkoani Njombe kwa siku zaidi ya tatu akipatiwa
matibabu mzazi wake.
Wanafunzi wakiwa nje ya shule yao ya Mbogamo Commerce Secondary School
Baada
ya mwandishi wa habari kufika katika Hospitali ya kibena ya mkoani
Njombe ambapo mwanafunzi mwanafunzi huyo amelazwa,Uongozi wa Hospital
hiyo umesema kuwa umezuiliwa kuzungumzia taarifa hiyo kutokana na
suala hilo lipo chini ya vyombo vya usalama.
Mkuu
wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akiongea na East Afrika Radio kwa
njia ya simu amekiri kutokea kwa tukio hilo wilayani kwake licha ya
yeye kuwa mbali ofisi amesema ni kweli mwanafunzi huyo alikutwa na
kosa lakini sheria iliyotumika kumuadhibu ni kinyume cha sheria
zilizowekwa na serikali.
Kituo
hiki kilifika shuleni hapo na kubaini kutokuwepo kwa walimu hao na
kuthibitika kuwa wanashikiliwa na vyombo vya usalama huku shule hiyoi
ikiwabakiwa na mwalimu mmoja tu kutokana na tukio hilo.

No comments:
Post a Comment