Serikali imesema kuwa
hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeiimarika hadi kufikia asilimia
80 ikiwa ni kutokana na ongezeko la fedha zilizopelekwa Bohari Kuu ya
Dawa, (MSD), ili kuviwezesha vituo vya afya vya umma nchini kupata
mahitaji yake ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Akizungumza leo Bungeni
Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dk. Hamis Kingwangalla amesema hali hiyo imetokana na
serikali kuongeza bajeti dawa kutoka shilingi bilioni 31 hadi kufikia
bilioni 251.5 katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Dkt. Kigwangala amesema
kuwa changamoto iliyokuwepo hapo awaloi ni kutokana na mfumo uliokua
unatumika katika usambazaji kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa
fedha lakini kwa sasa tatizo hilo linaelekea kumalizika kutokana na
kuongezewa bajeti ya dawa kwa wizara.
Aidha Naibu Waziri huyo
amewataka wabunge na viongozi wengine kushirikiana na Wizara hiyo
katika kupata taarifa juu ya wizi wa dawa katika vituo vya afya
kutokana na mfumo uliopo sasa kutoka mianya ya wizi huo wa dawa
katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:
Post a Comment